Kindy katika Mji wa Queensland (Swahili)

Kindy ni nini?

Mfumo wa shule za watoto uitwao Kindergarten unajulikana kwa jina la Kindy katika mji wa Queensland. Kindy ni programu ya elimu inayotolewa kwa watoto wadogo mwaka mmoja kabla ya kujiunga na shule. Kumwingiza mwanao katika programu ya kindy humfanya ajifunze kwa njia ya michezo, kuwa na marafiki na kujiandaa kujiunga na shule.

Programu za kindy zilizopewa ithibati na Queensland Government ziko katika mfumo wa michezo na hutolewa na walimu waliofuzu kufundisha watoto wadogo. Programu za kindy hutolewa katika vituo vya kulelea watoto wadogo; katika baadhi ya shule zilizoko mbali na mji; na kwa njia ya elimu masafa au kwa eKindy kwa baadhi ya wanafunzi ambao hawawezi kufika vituoni.

Jinsi watoto wanavyojifunza kwenye programu ya kindy

Katika programu hii ya kindy, watoto hujifunza mambo yafuatayo kwa njia ya michezo:

 • kutumia lugha kuwasilisha mawazo na hisia zao
 • kutengeneza marafiki, kushirikiana na kucheza na wengine
 • kujifunza kupitia uzoefu mpya
 • kujifunza kujiamini na kuwa mwenye nguvu
 • kuweza kujieleza kupitia sanaa, muziki na maigizo
 • Kukomaza na kuboresha maarifa waliyo nayo, kuwafanya wawe na uwezo wa kufikiri mawazo mapya na kuwasaidia wafurahie mwanzo mzuri wa shule.

Namna ya kujiunga na kindy

Ukiwa Queensland, watoto wanaweza kujiunga na kindy mwaka mmoja kabla ya kuanza shule. Kila kituo kina utaratibu wake tofauti wa kutoa huduma hiyo, ndio maana wengine hulazimika kusubiria kwa muda fulani. Kwa hivyo unashauriwa kuwasiliana na kituo cha kindergarten ulichokichagua juu ya muda muafaka wa kumwandikisha mtoto wako.

Mtoto wako anatakiwa awe ametimiza miaka 4 inapofikia Juni 30 ili aweze kuandikishwa kwenye kindy.

Tarehe ya Mtoto Kuzaliwa Mwaka wa mtoto Kujiunga na kindy
Kuanzia Julai 1 2013 hadi Juni 30 2014 2018
Kuanzia Julai 1 2014 hadi Juni 30 2015 2019
Kuanzia Julai 1 2015 hadi Juni 30 2016 2020
Kuanzia Julai 1 2016 hadi Juni 30 2017 2021
Kuanzia Julai 1 2017 hadi Juni 30 2018 2022
Kuanzia Julai 1 2018 hadi Juni 30 2019 2023

Mahitaji ya kumwandikisha mtoto wako:

 • jina la mtoto na anwani
 • taarifa zako kama mzazi wake, au mlezi
 • maelekezo ya mahakama yoyote au malekezo ya wazazi au mipango ya wazazi juu ya mwanao.
 • taarifa za mahitaji maalum (mfano ulemavu, vyakula ambavyo mtoto akila anadhurika au mahitaji mengine)
 • uthibitisho wa tarehe ya kuzaliwa (mfano cheti cha kuzaliwa)
 • afya na hali ya chanjo
 • taarifa za watu wanaoruhusiwa kumchukua mtoto wako na mtu wa kuwasiliana naye wakati wa dharura Kituo kinatambua taarifa hizi ni siri, kwa hivyo kitazitunza ipasavyo na utakuwa huru kupata taarifa zote za mwanao.

Kuchagua programu ya kindy

Watoto wote Queensland wana sifa ya kujiunga na kindergarten iliyosajiliwa mwaka mmoja kabla ya kuanza shule.

Kindergarten iliyosajiliwa huzingatia miongozo ifuatayo ya serikali:

 • programu ya elimu ya watoto wadogo kwa njia ya michezo inatakiwa iratibiwe na walimu waliofuzu kufundisha watoto wadogo kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya serikali
 • muda wa programu hiyo unatakiwa kuwa saa 15 kwa wiki, wiki 40 kwa mwaka, ambapo mtoto anatakiwa ajiunge na programu hiyo mwaka mmoja kabla ya kuanza shule.
 • Miongozo hiyo inaenda Sambamba na Queensland Kindergarten Learning Guideline au programu zingine zilizothibitishwa na Queensland Curriculum and Assessment Authority.

Ili kupata msaada wa kutambua programu za Queensland Government zilizopitishwa, angalia ‘kindytick’.

Kindy tick

Gharama za kindy

Ada za Kindergarten hutofautiana kati ya kituo kimoja na kingine. Wasiliana na kituo chako cha kindy ulichokichagua ili kupata taarifa za ada zao.

Punguzo au msamaha wa ada za Kindergarten hutolewa kwa familia zinazostahili, zikiwemo familia zisizo na wazazi ambazo husimamiwa na walezi tu. Familia hizo zinatakiwa kutimiza vigezo vifuatavyo:

 • Wawe na Health Care Card (HCC) ya serikali ya Australia iliyotolewa hivi karibuni (au awe nayo mtoto mwenyewe)
 • wawe na Australian Government Pensioner Concession Card (automatic HCC entitlements)
 • wawe na Department of Veterans’ Affairs Gold Card au White Card
 • wafanye mawasiliano rasmi, mfano barua, kutoka mamlaka husika kuonesha nia ya kupewa HCC
 • wanatakiwa wawe wazawa/wamezaliwa Australia (au uwe na mtoto mwenye sifa hiyo)
 • awe ni mtu mwenye familia ya watoto watatu au zaidi wenye umri sawa, waliojiunga na Kindy mwaka mmoja.

Ruzuku kwa waliopunguziwa au waliosamehewa gharama za kindergarten hutolewa moja kwa moja kwa vituo vinavyotoa huduma. Utaratibu huu unakusaidia kukupunguzia gharama ya kuwalea watoto wako. Hii inatolewa mara moja tu, hata kama una sifa kadhaa za kustahili.

Familia zenye watoto wanaohudhuria programu ya kindergarten muda mrefu kwa siku wanaweza pia kuwa na sifa za kupata Commonwealth Government Child Care Subsidy. Taarifa kuhusu kustahili kupata ruzuku za Commonwealth Government hupatikana katika Centrelink.

Watoto walio katika vituo vya malezi au wanaolelewa na ndugu wanaweza pia kupewa ruzuku ya nyongeza. Wasiliana na kindy na Child Safety Service Centre kwa taarifa zaidi.

Kwa taarifa zaidi

Wasiliana na Queensland Government kwa simu namba 13 74 68
Tafuta ‘kindy’ kwenye tovuti hii www.qld.gov.au/earlyyearscount

Published — 07 July 2016 Last updated — 18 March 2019

Want personalised tips and activities?

Complete these short questions to get personalised tips and activities to see how simple and easy it can be.

Get started
01 / 05

What is your relationship with the child?

MotherFatherGrandmotherGrandfatherCarer/Guardian

What best describes your location?

Metro
Regional
Remote

If you had a spare moment, what would you most likely do with the child?

Metro
Regional
Remote

And finally…

Do you speak another language at home apart from English?
Are you of Aboriginal and / or Torres Strait Islander descent?
Does the child need additional support with their development or learning?
Now we know a little more about the content that might interest you we’ve compiled it into a handy page for you.
Go